|
Wema Sepetu |
MSANII gumzo wa tasnia ya filamu bongo na miss tanzania pekee mwenye
nyota kali ya kupendwa kuliko maelezo, Wema Sepetu, ameuambia mtandao wa
DarTalk, kuwa hawezi kuolewa Tanzania kwani hata akiamua kuchukua
maamuzi hayo bado kuna watu wanaweza kumuharibia ndoa yake kwa sababu
zao binafsi.
Msanii huyo alidai kuwa hawezi kuacha kuzungumza ukweli kwani watu
hawapendi maisha yake na ndiyo maana kila siku hawaishiwi cha kusema juu
yake na hata mahusiano yake ya kimapenzi.
Alidai kuwa kutokana na kuandamwa na skendo kadhaa wanaume wengi
wanamini yeye ni mwanamke muhuni, na ndiyo maana hakuna anayetaka
kumchumbia, hivyo anaamini hawezi kuvishwa pete na mwanaume wa
kitanzania kwani tayari wameshalishwa maneno machafu juu yake.
“Unajua wapo watu ambao kazi yao ni kunichafua na hawapendi maendeleo
yangu, na kwangu mimi naamini hata kama nikisema nataka kuolewa kuna
watu watafanya juu na chini ili tu ndoa yangu isifungwe, hivyo naweza
kufunga ndoa na mwanaume wa nchi za nje kwani hata mi mwenyewe sitaki
wabongo,” alidai.
Mwandishi wa DarTalk, alipotaka kujua mahusiano yake na Diamond mwisho
wake utakuwa vipi, alijibu “Suala la mimi na Diamond halihusiani na
ishu yangu ya kufunga ndoa na mwanaume wa nje kwani najua Diamond hawezi
kuishi na mimi kwa sababu tayari naye anaanza kulishwa maneno kuwa
anatembea na mwanamke mkubwa wakati miaka yangu ni midogo sana,” alidai.
Hata hivyo mtandao huo ulipotaka kujua kauli ya Diamond juu ya Wema
anaposema kuwa hawezi kuolewa na mwanaume wa kibongo, hivyo kwa upande
wake anazungumziaje, lakini simu yake haikuweza kupokelewa baada ya
kuita kwa muda mrefu. |
|
|
|
No comments:
Post a Comment