Baada ya kuhojiwa na polisi kwa masaa nane, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ali Kiba.
Alipohojiwa na Soudy Brown, T.I.D alifunguka na kusema “kwa nini nimuue Ali Kiba bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo, kwa sababu gani?
Toka nimezaliwa sijawahi kugombana na Ali Kiba, ukibisha muulize mwenyewe kama ameshawahi kukorofishana na mimi, nia ya hao watu ni kuniangusha mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe.”
Soudy alipomtafuta meneja wa Ali Kiba alijibiwa “hakuna taarifa zozote ambazo ziko tayari kutolewa kwenye vyombo vya habari sasa hivi lakini ikiwa tayari utakua wa kwanza kujua”
SOURCE
No comments:
Post a Comment