Kambini wanaingia tarehe 30 August 2012, movie wanaanza kucheza tarehe 3 septemba inaitwa Nasikia kuitwa ambapo watakaocheza ni mdogo wake Kanumba kwa upande wa baba aitwae Mjanaheri pamoja na baba mzazi ambapo itachezwa hukohuko Shinyanga.
Movie imetungwa na Mwalimu Emanuel Yahewa ambae ni ndio msimamizi wa kikundi cha Taisee art kilichopo chini ya kanisa la AICT Kambarage ambapo Marehemu ndipo alikua anaimbia kwaya, alijifunzia gitaa na uigizaji hapo hapo.
Mwanzilishi wa kikundi hicho chenye watu 39 ni Mjanaheri Kanumba ambae amesema movie itakua imekamilika ndani ya mwezi mmoja, kampuni inayoitengeneza ni RJ ya Ray Vicent Kigosi lakini director ni Magulu ambae alikua Director wa Kanumba kwa miaka saba lakini kampuni ya Kanumba haitohusika hata kidogo na utengenezaji wa movie hiyo, baba mzazi wa Marehemu Kanumba atashiriki kucheza pia kama kiongozi wa sungusungu.
Stori yake haihusiani sana na maisha ya Kanumba japo mwishoni mwa hiyo movie kuna baadhi ya vitu vyake vitahusishwa, zikiwemo nyimbo na sehemu kidogo ya maisha yake.
Mwezi mmoja baada ya kifo cha Kanumba nilipata nafasi ya kufanya interview na familia yake Shinyanga, wadogo zake wanne walinihakikishia kwamba wako tayari kuingia kwenye soko la movie Tanzania kwa sababu uwezo wanao na wanataka kuliendeleza jina la ukoo wao.
No comments:
Post a Comment