|
Prezzo and Goldie |
Safari ya Prezzo nchini Nigeria imemrudisha bila kukipata kile
alichokiendea baada ya Goldie kuonekana kutofurahishwa na ziara yake.
Prezzo aliyekuwa mshindi wa pili kwenye Big Brother Africa StarGame wiki
hii alienda nchini Nigeria kuwaomba radhi wananchi wa huko na pia
kutangaza nia ya kumfanya Goldie awe mke wake. Katika mahojiano na
waandishi wa habari jijini Lagos, Prezzo alisema alienda nchini humo
kumuomba uchumba Goldie. Hata hivyo hakufanikiwa kuonana Goldie ambaye
Prezzo alisema hakuwa anapokea simu yake.
No comments:
Post a Comment