JESHI
la Polisi Mkoani Mbeya limesema halitaruhusu mikusanyiko ya mikutano ya hadhara
kwa vyama vya siasa wakati zoezi la sensa ya kuhesabu watu na makazi
linaloendelea mkoani hapa na kuwa chama chochote cha siasa kitakacho kiuka
agizo hilo hatua kali za sheria
zitachukua mkondo wake.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwan Athuman
wakati akizungumza na waandishi habari kuhusiana na na baadhi ya vyama vya
siasa kuendesha mikutano katika maeneo mengine hapa nchini. Kamanda Diwani amesema
kitendo cha baadhi ya vyama vya siasa kuendesha mikutano ya kisiasa kwa baadhi
ya maeneo hapa nchini wakati zoezi la sensa likiendelea inaweza kuathili
mwenendo mzima wa zoezi hilo ambalo linamanufaa kwa watanzania wote. Aidha amesema
kuna baadhi ya wanasiasa ambao wamekwenda katika ofisi yake kwa lengo la kuomba
kibali cha mikutano ya kisiasa,ambapo amejitahidi kuwaelewesha juu ya umhimu wa zoezi hilo kwa
masrahi ya taifa. Hata hivyo Diwani amesema
jeshi la polisi halipo tayari kuwafumbia macho wanasiasa ambao watakiuka
utaratibu huo ambao unalenga kulinda zoezi hilo la sensa kutoathiliwa na
mikutano hiyo ya hadhara ambayo inaweza kuchochea vulugu miongoni mwa wananchi
kwa kushindwa kuhesabiwa ipasavyo. Pia ameongeza kuwa kitendo hicho kitaharibu
utaratibu wa serikali wa kufanikisha zoezi la kupata takwimu sahihi kwa kila
mtanzania kwa ajili ya kuiwezesha serikali kupanga mipango ya miradi ya
maendeleo ya wananchi ambayo itakuwa na iwiano uliosawa. Kamanda huyo amebaishisha
kuwa mpaka sasa zoezi la kuhesabu watu na makazi linaendelea vizuri mkoani hapa
kwa kuwa hakuna malalamiko yoyote jitokeza na kuwa jeshi hilo limeimarisha
ulinzi wa kutosha kwa maeneo yote mkoani humo. Baadhi ya wananchi mkoani Mbeya kwa sharti la kutokutajwa majina ,wamekasirishwa
na kitendo cha baadhi ya wanasiasa kuendesha mikutano ya hadhara kwa baadhi ya
mikoa ambayo inachochea na kuleta vulugu wakati zoezi la sensa likiendelea kwa
nchi nzima. Wamesema zoezi la sensa ni la manufaa kwa watanzania wote bila ya
kujali itikadi za siasa na dini kwa kuwa
linaiwezesha serikali iliyopo madarakani kutekeleza malengo yake kwa ufanisi.
No comments:
Post a Comment