• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Tuesday, August 28, 2012

    “NIMERUDI NYUMBANI KUPUMZIKA NA SI KUTAFUTA MUME” – RAY C…!!


    BAADA ya kukaa nchini Kenya kwa muda mrefu na kurekodi ngoma kadhaa ikiwemo ‘Motomoto’, ‘Karibu Tanzania’ na nyingine kibao msanii
    Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema kuwa amerudi Tanzania kikazi na kupumzika na si kutafuta mume kama baadhi ya watu walivyodai.

    Hata hivyo msanii huyo alisema kuwa ngoma zake alizofanyia kazi zinafanya vizuri na mashabiki wake wa nchini Kenya wamekuwa wakimpa sapoti kubwa pale anapokuwa akifanya show.


    Rehema katika pozi


    Ray C alisema kuwa mwishoni mwamwezi huu anatarajia kuachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la ‘Moyo Waniuma’, ambayo itakuwa inazungumzia mambo mengi juu ya mapenzi.


    “Nimerudi bongo lakini si kutafuta mume kama watu wengi wanavyodai, bali nimekuja kwa ajili ya kazi zangu za muziki, pia nimekuja kumpumzika kwani nilikuwa nje kwa muda mrefu sana,”
    alisema Ray C.

    Aliongeza kuwa anaomba kuwaambia mashabiki wake kuwa bado hajaolewa na mambo yake yakiwa tayari juu ya kuolewa ataweka kila kitu wazi.

    No comments:

    3500K