• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Tuesday, August 28, 2012

    MWANA FA ATARAJIWA KUTOA BURUDANI YA NGUVU KATIKA FAINALI ZA SHINDANO LA FREESTYLE LA NOKIA




    Rapper wa Tanzania, Hamis Mwinjuma aka MwanaFA anatarajiwa kutumbuiza kwenye fanaili za shindano la freestyle la kampuni ya simu Nokia liitwalo Nokia Don’t Break the Beat.


    Fainali hizo zitafanyika Jumamosi hii ya September 1 jijini

    Nairobi, Kenya pande za Club Ichonic (zamani Club Barn) kuanzia saa 2 usiku huu.

    Wasanii wengine watakaotumbuiza ni Bamboo, Keko, Madtraxx, Octopizzo na STL.


    Mshindi wa kwanza kwenye shindano hilo atajishindia shilingi milioni 5 za Tanzania.


    Pamoja na zawadi hiyo mshindi wa kwanza atakula shavu la kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Decimal Media/Universal Records.


    Mkataba huo utamfanya mshindi arekodi nyimbo na kufanya video tatu katika kipindi cha mwaka mmoja huku kwenye video moja akifanya collabo na rapper wa kike Stella Mwangi, STL.


    Tangu mwezi uliopita msako wa kumpata mkali wa michano Afrika Mashariki umeendelea kwa kuzunguka kwenye miji ya Nairobi, Mombasa, Kisumu, Eldoret, Kampala na Dar-es-Salaam.

    No comments:

    3500K