IMEELEZWA kuwa, dola yoyote duniani,
haiwezi kupata ufanisi bila ya kuwepo ushirikiano mzuri miongini mwa wanajamii
husika.
Kauli
hiyo imetolewa na Richard Rimo, mjumbe wa tume ya kukusanya maoni juu ya rasimu
ya kuundwa kwa Katiba mpya ya Tanzania
wakati akizungumza na wakaazi wa shehia ya Kibuteni Mkoa wa Kusini Unguja. Rimo
amewataka wakaazi wa shehia ya Kibuteni kutoa maoni yao kwa uwazi zaidi ili kufikia lengo la
kuundwa kwa tume hiyo, sambamba na kuwahakikishia kuwa watayafanyia kazi kadiri
itavyowezekana.
Mapema
akitoa ufafanuzi, Mwenyekiti wa mjadala katika mkutano huo Muhammed Yussuf
Mshamba alisema kuwa mchakato wa Katiba ni muhimu sana kwani maoni hayo yataonesha kuwa
wananchi ndio wamiliki wa katiba hiyo. Aidha alisema Tume ya mabadiliko ni huru
na haiwazuii wananchi kutoa maoni yao kwani ndio
lengo la kuundwa kwake, lakini aliwaomba kuzingatia sana heshima ili waweze kufikia lengo
linalokusudiwa.
Miongoni
mwa wachangiaji, Rajab Haji aliiambia Tume hiyo kuwa Katiba itakayoundwa
izingatie haja ya kuwa na wagombea binafsi wa Ubunge, Udiwani na Uwakilishi na
kuondokana utaratibu wa sasa wa kutoa fursa kwa wagombea wenye vyama vya siasa
tu sambamba na kuvitambua vikosi vya SMZ.
Pia
alishauri Katiba ijayo izingatie kuwepo kwa mamlaka ya Watu wa Zanzibar
na ile ya Tanganyika huru,
pamoja na kutaka mgawanyo wa misaada kutoka nje itolewe sawa bila
kuangalia
ukubwa wa Tanzania
bara. Aidha Haji alitaka Katiba mpya itoe umuhimu katika masuala ya
elimu ya
juu, Mafuta na gesi, akishauri kila upande wa muungano uwe na haki ya
kuwa na
mamlaka yake, jambo litakalotoa nafasi kuwepo kwa mamlaka ya Watu wa
Zanzibar, na kutambuliwa hadhi ya Rais wa Zanzibar popote aendapo.
Mchangiaji
Pandu Haji ( 48 ), alishauri kuwa Katiba mpya izingatie kuwa Tanzania ni
Muungano wa nchi mbili hivyo ni vyema suala la ukusanyaji wa kodi liundiwe
taratibu mpya kwa TRA kufanya kazi zake Tanzania bara pekee na sio Zanzibar.
Hiyo, alisema itaipa mamlaka Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), kufanya kazi ya
kukusanya mapato kwa uhuru ili yainufaishe Serikali ya Zanzibar na kuinua uchumi wake.
No comments:
Post a Comment