Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania Eng. Suleiman s.
Suleiman akiwa na Mh. mwakyembe wakati alipofanya ziara ya kukagua
kiwanja cha ndege cha Arusha na kilimanjaro na baadae kuzindua bodi ya
ushauri ya KADCO.
akitoa
maelekezo kwa Mheshimiwa Waziri wa Uchukuzi dr. mwakyembe,Eng. Suleiman
alisema kuwa kiwanja hicho cha arusha kilisimama kupokea ndege kubwa
kutokana na ukarabati uliokuwa ukifanyika wa barabara ya kuruka na kutua
ndege ambao kwa sasa umekamilika na shirika la ndege la Precision
litaanza kutua kiwanjani apo kuanzia mwanzoni mwa July 01 2012.
Aidha
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege alieleza kuwa, mamlaka
ya viwanja vya ndege katika mipango yake ya muda mfupi inatarajia
kujenga maegesho mapya ya ndege,kujenga jengo jipya la abiria,kurefusha
barabara ya kutua na kurukia ndege ili ifikie urefu wa meta 1800 na
upana wa meta 30 na kujenga barabara ya kiungio yaani parrarel tax way.
No comments:
Post a Comment