Katibu
Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego akisisitiza jambo wakati
akihitimisha mjadala kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki
makao makuu ya BASATA.Wengine kulia ni Mhandishi Joel Chacha kutoka
malaka ya mawasiliano nchini (Tcra) na Kaimu Mratibu wa Jukwaa hilo
Agnes Kimwaga.
Na Mwandishi Wetu
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kujipanga kwa ajili ya
kuhimili ushindani wa kimataifa kutokana na ujio wa mfumo wa digitali
ambao utazifanya kazi zao kuonekana kimataifa.
Wito
huo umetolewa wiki hii kwenye ukumbi wa BASATA na Katibu Mtendaji wa
baraza hilo, Ghonche Materego wakati akihitimisha mjadala kwenye Jukwaa
la Sanaa uliohusu Teknolojia ya Digital na Faida Zake Katika Sekta ya Sanaa uliochokozwa na Mhandisi Joel Chacha kutoka mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tcra).
Alisema
kuwa, mfumo wa digitali utaruhusu uwepo wa vituo vingi vya redio na
runinga ambavyo vitakuwa na masafa ya kimataifa hivyo ni wazi wasanii
wanatakiwa kujipanga katika kuandaa maudhui bora, ya kutosha na yenye
mvuto kwa ajili ya kukidhi ongezeko hilo na zaidi ushindani wa
kimataifa.
“Wasanii
tujipange, fursa zinazokuja ni nyingi mno, zinahitaji maudhui ya
kutosha, yenye ubora na yatakayoweza kuvifanya vyombo vya habari viweze
kuhimili ushindani pia” alisisitiza Materego.
Aliongeza
kuwa, moja ya eneo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wamiliki wa vyombo
vya habari ni uhafifu wa maudhui ya kazi za Sanaa hivyo, wasanii hawana
budi kuacha kulalamika na kujipanga kukabili changamoto hiyo.
Awali
akiwasilisha mada hiyo,Mhandisi Chacha alisema kuwa, mfumo wa digitali
utazalisha fursa nyingi katika sekta ya Sanaa lakini akasisitiza kuwa,
uchangamfu wa Wasanii wetu ndiyo utawafanya wafaidi.
Alizitaja
baadhi ya fursa hizo kuwa ni pamoja na; ongezeko la ajira kwa Wasanii,
ongezeko la vipindi, kukua kwa ushindani katika ubunifu na utengenezaji
maudhui yenye ubora, Sanaa za Tanzania kutangazika kimataifa na
kuongezeka kwa makampuni yatakayojihusisha na sekta ya Sanaa
“Mfumo
wa digitali una mazuri mengi lakini kubwa ni kuongezeka ushindani na
ubora katika kutengeneza maudhui yenye ubora na pia ongezeko la masafa
katika televisheni ambayo yatahitaji maudhui (vipindi) ya kutosha”
Aliongeza Chacha.
Hata
hivyo, aliitaja changamoto ya uharamia kwenye sekta ya Sanaa ambapo
aliwashaiuri wasanii kuamka na kujiunga na Chama cha hakimiliki (Cosota)
ili kuhakikisha kazi zao zinalindwa kisheria.
Wadau
wengi waliochangia mjadala huo walionekana kuwa na wasiwasi na mfumo wa
digitali lakini wakaomba elimu ya kutosha itolewe ili wananchi wengi
zaidi waelewe nini maana ya kutoka mfumo wa analogia kwenga ule wa
digitali
No comments:
Post a Comment