Pamoja na kwamba aliapa hatorudi tena Dar ni bora aende kuishi kwao Arusha baada kutoridhika na vitu alivyokua akifanyiwa na Meneja Madee wa Tip Top Connection, Dogo Janja ametangaza kurudi Dar ijumaa ya leo June 22 2012.
Exclusive na AMPLIFAYA Janja ambae amemaliza wiki moja toka arudi kwao Arusha, amesema “namshukuru Mungu amesikia kilio changu na nakuja kucheki mikataba ya kujiunga na kundi la WATANASHATI kwa Ostaz Juma na kama nitaridhika na mikataba nitajiunga nao, nimekaa na wazazi wameniambia zile zilikua hasira tu nirudi Dar es salaam kusoma na kufanya muziki kweli nikakaa nikajifikiria nikaona ni sawa”
.
No comments:
Post a Comment