MISS UTALII TANZANIA 2005 ,KILY JANGA BAADA YA KUSHINDA TAJI LA DUANIA LA MISS TOURISM WORLD SADIC 2006, HUKO CHINA
·
Sasa ni Taasisi ya Kutangaza na kuhamasisha Utalii, Utamaduni, Bidhaa
za Ndani,Utalii wa Ndani,Utalii wa Kitamaduni,Utalii wa Michezo na
Utalii wa Mikutano, Mazingira,Elimu,Afya ya Jamii,Kilimo, Madini na
Maliasili kitaida na kimataifa.
·
Vitengo vya Miss Tourism Tanzania International, National Parks
Marathon, Tanzania Great Safari & Tour, Tanzania Beach Soccer na
Tanzania Cultural Carnival, Festival & Conference vyaanzishwa.
·
Fainali na Uongozi Ngazi za Majimbo, Wilaya, Mikoa, Mikoa
maalumu ya Vyuo Vikuu, Kanda, Kanda maalumu za Vyuo Vikuu na Taifa.
·
Waandaaji,Viongozi na washiriki mamaluki 40 yao imefika, Kila
Mbunge, Mkuu wa Wilaya,Mkuu wa Mkoa kuwa na Miss /Binti Utalii katika
jimbo lake
· Kuswahili sasa Lugha Rasmi ya Mashindano hayam wawakilishi katika mashindano ya dunia kutumia Kiswahili jukwaani.
· Wakaribisha mawakala wapya, na kuwataka wa zamani kuomba upya.
Bodi
ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania, imeanza kuonyesha cheche zake
kwa kishindo, kwa kufumua mfumo mzima wa uongozi na mashindano haya
makubwa na yenye mafanikio nchini.Katika kikao chake kilichofanyika
mwishoni mwa wiki,chini ya makamu mwenye kiti wa bodi hiyo Ndugu Abubari
Omari Abubakari, bodi imechukua hatua mbalimbali kwa lengo la kuboresha
na kimarisha Mashindano haya lenye manufaa makubwa kiuchumi,kitamaduni
na kijamii kitaifa na kimataifa.
Bodi
imeazimoa kuchukua hatua katika Nyanja mbalimbali za mashindano haya,
kuanzia mfumo wa mashindano,uongozi,utawala na uendeshaji mzima wa
mashindano. Bodi imeazimia kufanya mabadiliko haya, na kuwa Miss Tourism
Tanzania Organisation, ni taasisi ambayo kuanzia sasa itaendeshwa kwa
mfumo wa kitaasisi, ambayo sasa badala ya kuwa taasisi ya mashindano ya
urembo pekee, inakuwa ni taasisi ya kuhamasisha na kutangaza Utalii,
Utamaduni, Mazingira, Elimu, Afya ya Jamii, Bidhaa za Tanzania, Uvuvi,
Wanyama Pori, Madini, Hifadhi za Bahari, sera za Taifa za Utalii,
Utamaduni, Kilimo, Mazingira, Umasikini, Vijana, Wanawake na watoto,
Utalii wa Ndani,Utalii wa Kitamaduni, Utalii wa Michezo na Utalii wa
Mikutano.
Pia
kupiga vita Uvuvi haramu, Uwindaji Haramu, Umasikini, Maradhi, Ujinga,
Tamaduni kongwe na Potifu kitaifa na kimataifa.Malengo haya yatafikiwa
kupitia mashindano ya Miss /Binti Utalii Tanzania, Miss tourism Tanzania
International, Miss Tourism University World, Miss Heritage World,
Tanzania Beauty and Model Management, National Parks Marathon, Tanzania
Great Safari and Tour na Tanzania Cultural Carnival and Festival kila
mwaka.
Aidha
kuanzia mwaka huu, pamoja na Shindano la kitaifa la Miss Utalii
Tanzania, fainali za Taifa zitakwenda sambamba na Miss Tourism Tanzani
International, ambapo washiriki wa Tanzania watapanda jukwaani kuwania
taji la taifa sambamba na washiriki waalikwa kutoka nchi mbalimbali
Duniani wakiwania taji la Miss Tourism Tanzania International,ambapo
washindi wake watakuwa mabalozi wa Tanzania katika mabra na nchi zao.
Kwa
kuwa na washiriki kutoka katika mabara yote duniani ikiwemo
Ulaya,Marekani,Asia,India,Marekani Kusini,Afrika na Urusi Shindano la
Miss Utalii Tanzania sasa litakuwa ni la kimataifa na lenye uwezo mkubwa
wa kuitangaza Tanzania, Utalii ,Utamaduni na mali asili zake kimataifa,
kwani fainali za taifa kuanzia mwaka huu, zitaonyeshwa LIVE duniani
kote kupitia Televisheni na mitandao ya Internet. Bodi pia imepitisha
azimio la kutumia lugha ya Kiswahili kwa wawakilishi wote wa mashindano
haya katika mashindano ya dunia na mengine ya kimataifa, ili kukitangaza
vyema Kiswahili ambayo ni lugha ya limataifa na ya Afrika, kama ambavyo
washiriki kutoka mataifa mengine wanavyo tumia lugha zao na kushinda
mataji ya Dunia.
Bodi
imefanya uchambuzi wa kina wa wakurugenzi na waandaaji wa ngazi
mbalimbali, na kupitisha azimio la kuwataka waandaaji wa Majimbo
(Vitongoji) ,Wilaya, Mikoa, Mikoa maalum ya Vyuo Vikuu, Kanda na Kanda
maalum za Vyuo Vikuu kuomba upya na kutoa fulsa kwa watu na makampuni
mbalimbali kuomba kuandaa katika ngazi yoyote nchini, isipokuwa
waandaaji wake katika mabano Dar es Salaam, Ilala na Temeke (Film
Directors Association) Katavi (KATABI CO. LTD & COUNTRY WIDE
ENTERTAINMENT) Arusha na Mara (NAMAN 201O LIMITED ),Tanga ( Kambi
Mbwana Entertainment),Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam ( ERIADO POINT
VIEW) Kanda ya Kusini (MOD INTERGRATED SOLUTION AND AWARENESS) na Kanda
ya Ziwa (FANIA BEAUTY ENTERTAINMENT) ambako waandaaji wake wanabaki kama
walivyo. Ambako waandaaji wapya wanatakiwa na wazamani wanaruhusiwa
kuomba ni:
1. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kaskazini, Mashariki, Mgharibi na Kati.
2. Miss Utalii Tanzania – Kanda za vyuo Vikuu – Kaskazini, Kusini, Kati, Magharibi, Ziwa na Mashariki.
3.
Miss Utalii Tanzania –Mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma,
Kagera, Rukwa, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mwanza, Ruvuma, Lindi, Mtwara,
Lindi, Pwani, Morogoro, Manyara, Kilimanjaro ,Iringa, Mbeya, Njombe.
4.
Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Mikoa ya Dodoma, Morogoro, Tanga,
Mwanza, Kagera, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Arusha na Tabora.
5. Miss Utalii Tanzania – Majimbo yote ya Wabunge na Wilaya.
Mwisho
wa kupokea maombi ya waandaaji wapya na wa zamani ni tarehe 12 Juni
2012, waombaji wanaweza kutuma maobi yao kupitia anuani zetu barua pepe
ambazo zina patikana katika website (www.misstourism/utaliitanzania.com,
blogspoti (misstourismorganisation.blogspot.com na mitandao yetu ya
facebook, twitter na Skype (misstourismtanzania au missutaliitanzania).
Kwa
mfumo huu mpya unalenga kufikisha kwa umakini na ustadi mkubwa Shindano
hili hadi ngazi za cheni kabisa za wananchi, na kufanya kila mbunge wa
jimbo , mkuu wa Wilaya, mkuu wa Mkoa na Rais wa nchi kuwa na mabalozi
wao wa Utalii kupotia mashindano haya, ambao watasaidia na kuwa na
jukumu la kuhamasisha Utalii, Utamaduni, Utalii wa Ndani, Utalii wa
kitamaduni, mazingira, Elimu, Afya ya Jamii, Kilimo, na Mianya ya
uwekezaji katika ngazi zao , sambamba na mamlaka za umma na binafsi za
ngazi hizo, huku wakitafsiri kwa vitendo sera husika za taifa. Aidha
bodia imeazimia kuimarisha umakani na kitengo cha uchunguzi na
intelijensia cha Shindano ili kubaini njama,hujuma na mamluki katika
Shindano hili, kabla hawaja leta madhara na kuwachukulia hatua kali
ikiwemo kuwafikisha katika Vyombo vya dola.
Akizungumza
na waandishi wa Habari, Abubakari alisema kuwa, pamoja na sababu za
kukosa umakini na ufanisi, waandaaji hao wa ngazi za mikoa na kanda
wamekuwa wakiruhusu warembo wasio na viwango na hata vigezo kushiriki
katika mashindano, jambo ambalo ni kinyume kabisa na kanuni na taratibu
za mashindano haya, ambayo kwa miaka mitano mfulizo yamekuwa yaki fanya
vyema katika mashindano mbalimbali ya Dunia na kimataifa.
“Tumelazimika
kuchukua hatua mapewa, ili kulinda hadhi ya mashindano haya kitaifa na
kimataifa. Ni mkakati wa bodi ya mashindano sasa kuwaondoa mashindanoni
washiriki wote ambao hawakidhi viwango bila kujali mataji watakayo kuwa
wametwaa katika ngazi zao. Fainali za Taifa mwaka 2012 zitafanyika mwezi
Novemba 2012 ,ili kutoa fuksa kwa waandaaji wa kanda na mikoa iliyo
salia kufanya fainali zao,pia kuzingatia kalenda mpya za mashindano ya
Dunia na kimataifa.
Asante,
Abubakari Omari Abubakari
Makamu Mwenyekiti Bodi ya Mashindano ya Miss/ Binti Utalii Tanzania
No comments:
Post a Comment