Baada
ya kuwa na bifu lililodumu toka mwaka 2006 hadi kufikia mwaka huu wa
2012 mastaa wawili kutoka pande za Obama wamekaa chini na kuamua
kulifutilia mbali bifu hilo na kuganga ya mbele. Bifu hilo lililoanza
mwaka 2006 baada ya 50 cent kumtukana Opra kwa kile alichodai kuwa
Mwanamama huyo ni mbaguzi kwani kwenye show yake inayorushwa na kituo
chake cha Luninga cha OWN amekuwa akiwabagua wasanii
weusi wa HipHop nakuwapendelea vibibi vizee vya kizunguu ambapo kutokana na upendeleo huo 50 Cent aliamua kumwita mbwa wake jina la Oprah kutokana na kumchukia mwanamama huyo, Lakini jana kupitia new Episode ya kipindi cha Oprah show wawili hao waliweza kukaa na kumaliza tofauti zao hizo.
No comments:
Post a Comment