• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Wednesday, December 10, 2014

    Bilionea wa Nigeria amzawadia Tayo $350,000 baada ya kuzikosa $300,000 za BBA HotShots


    Imeripotiwa kuwa baada ya mshiriki wa Nigeria kwenye shindano la Big Brother Afrika, Tayo kuzikosa dola laki tatu za Biggie zilizomwendea Idris wa Tanzania Jumapili iliyopita, mshiriki huyo wa Naija amezawadiwa $350,000 sawa na zaidi ya milioni 600 kutoka kwa shabiki wake bilionea.
    Idris (kushoto) akiwa na Tayo (kulia)
    Bilionea huyo aitwaye Ayiri Emami ameamua kuongeza dola 50,000 juu zaidi ya ile ambayo ilitolewa na Biggie ambayo ni $300,000 kutokana na kuwa shabiki mkubwa wa Tayo.
    Staa wa Nigeria Davido ameshare picha ya story hiyo Instagram na kuandika “we do this easy, bar dey” .
    Inasemekana hii si mara ya kwanza kwa bilionea huyo kumwaga mkwanja mrefu kwa wasanii anaowapenda, aliwahi kufanya hivyo kwenye harusi ya 2Face 2010 ambapo inasemekana alitoa zaidi ya Naira milioni 20 ( sawa na zaidi ya Tsh 189,000,000) na kumzawadia Range Rover mpya, na pia alimzawadia msanii mwingine aitwaye Durella gari aina ya Toyota Prado Jeep

    No comments:

    3500K