• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Tuesday, January 22, 2013

    WAWILI WAFA, MMOJA APIGWA RISASI NYUMBANI KWAKE HABARI KUTOKA KILIMANJARO


    NA JAIZMELALEO

    Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Kilimanjaro likiwemo tukio la mtu mmoja kupigwa risasi ubavuni na kufariki dunia papo hapo na watu wanao sadikiwa ni majambazi wilayani Hai.
    Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wapolisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, amesema kuwa tukio hilo limetokea hivi karibuni  katika eneo la Machame Wari wilayani hai.
    Boaz amesema kuwa awali kundi hilo la majambazi wapatao wanne walivamia kiosiki cha mfanyabiashara Emanuel Poul ambapo walifanikiwa kupora fedha zote za mauzo na kumpiga risasi Mustafa Ramadhani (45) na kufariki dunia papo hapo.
    Aidha kamanda Boaz amesema tukio hilo lilikuja siku chache baada ya kundi hilo la majambazi kumvamia mfanyabiashara  Matei Tumbo ambapo walifanikiwa kumpora bunduki yake  aina ya Short Gun na gari lenye nambari T264 ABY aina ya Toyota korola.
     Amesema kuwa majambazi hao walipora bunduki hiyo na kukimbia na gari hilo kabla ya kwenda kwenye uhalifu  na kumuua mfanyabiashara huyo .
    Boaz alisema kuwa katika tukio hilo jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watu wawili wanao sadikiwa kuhusika na tuki hilo ambapo waliwakuta wakiwa na risasi tatu za bunduki aina ya short Gun. Na kwamba uchunguzi unaendelea ili kuwabaini watu wengine.
    Katika tukio jingine kamanda boazi amesema kuwa januari 20 mwaka huu wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kuna mtu moja aliye julikana kwa jina moja la priscus alifariki dunia baada ya nyumba yake kuwaka moto.
    Amesema kuwa mtu huyo alifariki dunia baada ya chumba alichokuwa amelala kuteketea kwa moto na kwamba chanzo cha moto huo ni mshumaa alio kuwa amewasha  kuangukia godoro na kuwaka moto.

    No comments:

    3500K