• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Tuesday, January 1, 2013

    WAFA KWA KUGOMBEA MWANAMKE


    WANAUME wawili wamefariki dunia kwa kuchomwa visu na kupigwa na mawe katika tukio la kugombea mwanamke wilayani Tarime, Mara.
    Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya, Justus Kamugisha, alisema tukio hilo limetokea juzi kwenye eneo la gulio katika Kijiji cha Nyibaso, Tarafa ya Ingwe, wilayani Tarime.
    Alisema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi, ambapo wanaume hao walikuwa wakigombania mwanamke huyo ambaye ni mjane.
    Alisema katika tukio hilo, mwanamume aliyefahamika kwa jina moja la Nyamureba, mkazi wa Kijiji cha Matanka, wilayani Serengeti, alimshambulia Juma Mseti au Marwa (20), mkazi wa Kijiji cha Nyibaso kwa kumchoma na visu tumboni na kusababisha kifo chake papo hapo.
    Alisema baada ya kumuua mwenzake, mwanamume huyo alikimbia, ambapo wananchi wakiongozwa na ndugu wa marehemu, walimfukuza na kufanikiwa kumkamata na kumchoma visu na kumpiga kwa mawe hadi kumuua.
    Alisema kuwa mwanamke aliyekuwa anagombaniwa na wanaume hao ametoroka.
    CHANZO: Ahmed Makongo, TARIME

    No comments:

    3500K