• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, November 1, 2012

    Sintah Asema "Mwenye Picha zangu za Uchi Aziweke Mtandaoni Muone ujinga Wangu"

    NEWZ>>>FILEX MMARI 






    MSANII wa filamu ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha TV cha ‘Harusini na Sintah’ kitachorushwa DTV, Christine John ‘Sintah’, amekanusha vikali uwepo wa picha zake za utupu na kudai kuwa anayesema anazo basi aziweke hadharani ili watu waone ujinga wake ingawa anaamini kuwa katika maisha yake hajawahi kupiga picha za namna hiyo kama watoto wadogo wanavyofanya.

    Lipo kundi la watu kadhaa linalodai kuwa wana picha za msanii huyo zinazomuonesha mwili wake ukiwa mtupu kama alivyozaliwa huku ikidaiwa kuwa picha hizo alipigia nchini Marekani na baadhi yake zilitumika kwenye movie kadhaa za utupu.

    Habari juu ya ishu hii zilikuwepo chinichini lakini mwandishi wetu  akaona si vibaya akizungumza na muhusika ili kujua anazungumziaje, ambapo alidai kuwa anasikia watu wakisema kuwa wana picha zake za utupu lakini kwa upande wake anaamini katika maisha yake hajawahi kupiga picha za namna hiyo pengine apigwe na mpenzi wake bila yeye kujua.
    Alisema kuwa mara nyingi safari zake za nje huwa si kwa ajili ya kufanya upuuzi kama huo bali anaenda kwa ajili ya kazi hivyo baadhi ya watu wanaona wivu na ndiyo maana wanazusha habari ambazo hazileti picha nzuri kwani jamii.

    “Mimi ni jeshi la mtu mmoja hivyo wanapoona mafanikio yangu yanakuja wanaanza kuleta habari zao za kumchafua mtu, nawaambia tu kwamba sitishiki na nitazidi kusonga mbele na hao wanaosema hivyo watabaki na umaskini wao,” alisema.

    No comments:

    3500K