• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Monday, October 29, 2012

    Ommy Dimpoz Atangaza Kumsamehe Lord Eyez Kwa Namibia

    NEWZ>>>FILEX MMARI 




    Nyota wa muziki wa  kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz amesema kuwa licha ya kutumia kiasi cha  shilingi milioni 5 kurudisha gari yake kwenye hali ya kawaida hawezi kumchukia msanii mwenzake Lord Eyez anayeshikiliwa korokoroni hivi sasa kwa tuhuma za kuiba vifaa kutoka kwenye gari yake.

    Akizungumza na mtandao huu  mapema leo Ommy Dimpoz amefunguka kuwa ingawa kwa sasa haruhusiwi kusema lolote  kuhusu jambo hilo lakini anayo haki ya kusema kuwa binafsi amesamehe na anamuachia Mungu.

    “Nafahamu kuwa kuwa siruhusiwi kuzungumza lolote kwa kuwa suala liko Polisi,ninachoweza kukwambia  ni kuwa binafsi nimemsamehe Lord na wenzake, sababu huwezi kujua kuhusu kesho, nimepanga  kukutana naye na kumwambia hili jambo, najisikia vibaya lakini nashukuru kuwa gari yangu nimeshairekebisha na sasa ndiyo ninayoitumia tena licha ya kuwa nimetumiagharama kubwa” alisema Dimpoz.

    Katika hatua nyingine nyota huyo wa songi la ‘Badae’ ameanika kuwa wimbo huo umemuingizia kiasi kikubwa cha pesa tofauti na yalivyokuwa matarajio yake  huku pia akijikusanyia wingi wa marafiki ndani na nje ya nchi kupitia wimbo huo.

    No comments:

    3500K