• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Saturday, October 27, 2012

    MATONYA AELEZA JINSI ANAVYOKABILIWA NA IMANI ZA KISHIRIKINA KATIKA MAMBO YAKE.

    NEWZ>>>FILEX MMARI


    Kwa yeyote anaefatilia Bongofleva toka kitambo kidogo najua jina la MATONYA lazima litakua kwenye list ya familia ya wanabongofleva.
    Ni jina ambalo limekuwa kwenye vichwa vizito vya habari mara kadhaa kutokana na story kama ya kukamatwa na dawa za kulevya China pamoja na story nyingine.
    Story ya mwisho mimi kuisikia na

    nikawa na hamu ya kuifahamu ni kuhusu taarifa kwamba msanii huyu mzaliwa wa Tanga amekwama kwenye ishu zake za maendeleo kwa sababu kuna watu wanamloga asifanikiwe tena ikiwemo kukwamisha uzinduzi wa hotel yako aliyoijenga tanga ambayo ilitakiwa kufunguliwa toka miezi 6 iliyopita.
    Namkariri akisema
    "Nilikua na harakati hizo za kufungua hotel lakini majukumu yalinizidi nguvu kidogo lakini dhamila yangu iko palepale japo ile time niliyotarajia haikufanikiwa lakini bado nina mpango huo japo sitatoja siku, kuhusu ushirikina hiyo inasemekana lakini siwezi kusema ni kweli au sio kweli kwa sababu hayo ni mazingira ambayo yametuzunguka, mazingira yetu sisi waswahili.
    Siwezi kusemea swala hilo liko vipi lakini kikubwa tunapigana kila siku sichoki kumuomba mungu kwa sababu siku zote penye mazuri hakukosi kuwa na mabaya kwa hiyo yanayosemwa labda ni ya kweli au sio kweli".

    Hotel yake ni vyumba 10 ambapo ina pub ndani yake


    No comments:

    3500K