• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Wednesday, October 17, 2012

    HAWA NDIO WAUAJI WA WALE WANACHUO WANNE NIGERIA, WALIWACHOMA MOTO KWA TUHUMA ZA WIZI WAKATI SIO KWELI.

    Watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi.
    Ni wiki mbili zimepita lakini hii taarifa bado inaongoza kwenye headlines za Nigeria, ni kuhusu wanachuo wanne ambao walipigwa, waliteswa, walitembezwa uchi barabarani na baadae kuchomwa moto hadharani wakidaiwa kuwa ni wezi.
    Imefahamika ni watuhumiwa 13 akiwemo chief wa hicho kijiji cha Aluu ambae alihusika pia kuwachoma moto hao wanachuo.
    .
    Watuhumiwa hao wamesema kulikua na askari polisi mmoja ambae aliwaaambia wawachome moto hao wanachuo wakati huohuo kulikua na askari mwingine aliesema wasichomwe moto.
    Chanzo cha kuchomwa moto kilitokana na mmoja kati yao kuwaomba wenzake kumsindikiza kwa jamaa mmoja aliekua akimdai hapohapo kijijini lakini kibao kikawageukia baada ya jirani wa mdaiwa kuanza kupiga kelele kwamba wamevamiwa na wezi, vivyo hivyo kwa mdaiwa pia ambae alimuunga mkono jirani kwa kusema kweli wanachuo hao walikua wezi, wananchi wakakusanyika na kuanza kuwapiga.
    Kilichopelekea wananchi kutotoa nafasi ya kuwasikiliza wanachuo walipojitetea ni pamoja na mfululizo wa matukio ya uhalifu ambayo yamekua yakitokea kwenye hicho kijiji kwa siku za karibuni kwa wanakijiji mbalimbali kuibiwa.

    No comments:

    3500K