• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Tuesday, October 9, 2012

    Binti afanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne wodini baada ya kufanyiwa upasuaji

    Kuna watu kweli ni jembe. Nimempigia saluti huyu binti na mikono yote miwili kwa moyo na ujasiri. Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Alfa Germ, Morogoro, Jessica Kiliani (17), amefanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne akiwa wodini baada ya kufanyiwa upasuaji kwa zaidi ya masaa mawili na madaktari!

    Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Jessica kuomba aruhusiwe kufanya mtihani huo licha ya kuwa wodini akiugua kufuatia operesheni aliyofanyiwa na kulazwa katika wodi ya wazazi namba 7B.

    Mama mzazi wa Jessica, Anna Ngapemba alisema alipigiwa simu na mkuu wa shule saa 6:00 usiku Jumamosi iliyopita akimjulisha kuwa binti yake anasumbuliwa na tumbo na anahitaji msaada wa haraka. Mama wa Jessica alisema alienda shuleni hapo usiku huohuo na kukutana na mama mlezi (matron) wa hosteli za shule hiyo na kujulishwa juu ya hali ya binti yake na kwa kushirikiana na uongozi wa shule hiyo, walimpeleka katika Hospitali ya Mkoa.

    Alisema wauguzi waliokuwa hospitali usiku huo walimpigia simu daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, Christopher Manumbu. Dr Manumbu alipofika hospitalini hapo, alimfanyia Jessica upasuaji haraka kutokana na hali yake kuwa mbaya.

    Jessica licha ya kuwa katika hali ya maumivu alifanya mitihani miwili (Kiingereza na uraia) kama wenzake, katika wodi hiyo ya wazazi, akiwa chini ya msimamizi wa mitihani na polisi,

    Jessica alisema hakuwa tayari kuikosa mitihani hiyo na ndiyo maana alimwomba mama yake kuwasiliana na uongozi wa shule yake ili umwandalie mazingira mazuri ya kufanya mtihani akiwa wodini.

    No comments:

    3500K