• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Tuesday, October 16, 2012

    ASIA NEWS: MFALME SIHANOUK WA CAMBODIA AFARIKI DUNIA


    Kiongozi wa zamani wa   taifa la Cambodia Mwana mfalme Norodom Sihanouk  amefariki  mjini  akiwa  na  umri  wa miaka  89. 
    Naibu  waziri  mkuu  wa  Cambodia  Nhek Bun Chhay  amesema  kuwa  Sihanouk  amefariki  kutokana  na uginjwa  wa  moyo. Sihanouk  aliongoza   kampeni  kwa nchi  yake  kupata  uhuru  mwaka  1953  kutoka  Ufaransa , na  alichaguliwa   kuwa  mkuu  wa  nchi  mwaka  1960. Miaka  kumi  baadaye  aliangushwa  kutoka  madarakani katika  mapinduzi  yaliyoungwa  mkono  na  Marekani. Akiwa  uhamishoni   nchini  China  alijihusisha   na  kundi la  Khmer  Rouge,  na  baadaye  alihitilafiana  na  utawala huo  wa  kikomunist  wenye  msimamo  mkali,  na kuishi kwa miaka  12  zaidi  nchini  China. Alijivua  madaraka yake  ya  ufalme mwaka  2004  kutokana  na  afya  yake kuwa  mbaya.  Hivi sasa Mtoto  wake  mkubwa   , Norodom Sihamoni,  ndie  mfalme wa Cambodia.

    No comments:

    3500K