• Breaking News

  Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

  It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

  Thursday, September 13, 2012

  Wema Sepetu katika Balaa Lingine Tena..dahh


  Gari la Wema aina ya Toyota Mac X likiwa limekongolewa vioo vya pembeni.
  Musa Mateja, Dar es Salaam
  BEAUTIFUL Onyinye wa Bongo, Wema Isaac Sepetu, hivi karibuni alijikuta akipata wakati mgumu baada ya kukombwa vioo vya gari lake aina ya Toyota Mark X  na vibaka wa Moshi, Kilimanjaro, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili.
  Tukio hilo limetokea hivi karibuni ndani ya Viwanja vya Chuo cha Ushirika  ambapo staa huyo alikuwa amehudhuria uzinduzi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
  Akiwa katika burudani hizo, Wema  ambaye muda mwingi alionekana kuwa mtu mwenye furaha ghafla alibadilika na kuishiwa na furaha alipolikuta gari lake likiwa limekongolewa vioo vyote vya pembeni.
  Gazeti hili  lilizungumza na  Wema  kuhusu tukio hilo ambaye alionekana  kushangazwa  na tukio hilo na kusema kuwa  hakutarajia  kukutana nalo  kwa kuwa alikuwa  akiwaheshimu sana watu wa Moshi.
  “Imeniuma sana baada ya kukuta gari langu limekongolewa,  wameiba vioo na ukiangalia nipo ugenini, halafu magari ni mengi yaliyokuwa yamepaki uwanjani, kwa nini yasiibiwe hayo mengine wakaiba langu tu, dah! imenikera sana,” alisema Wema kwa uchungu.
  Hilo ni tukio lingine la Wema kulizwa, alishawahi kuibiwa nyumbani Sinza jijini Dar baada ya wezi kuruka ukuta na kumkomba baadhi ya vitu vya thamani, pia alishawahi kuibiwa vitu vingine ndani ya gari Uwanja wa Taifa.
  Post a Comment
  3500K