• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Friday, September 7, 2012

    Mke Alimzuia David Mwangosi(Marehemu) Asiende mkutanoni


     
    KIFO cha aliyekuwa mwakilishi wa Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi kilichodaiwa kusababishwa kwa kupigwa bomu na askari polisi Septemba 2, 2012, kimeanza kuzua mengine.
    Kwa mujibu wa rafiki wa karibu na marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la David, asubuhi ya siku ta tukio marehemu alimwambia anaweza asiende kwenye Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi kwenye ufunguzi wa tawi la Chadema kwa sababu mkewe. Itika Mwangosi amemzuia.
    “Siku hiyo kabla ya yeye kwenda Nyololo ilikuwa tukutane Ipogoro. Akanitumia meseji akisema anaweza asiende kwa sababu mkewe amemzuia akimpa sababu kwamba akienda watoto watammisi sana,” alisema rafiki huyo.
    Akaongeza: “Lakini baadaye akasema amefika Nyololo, ila hakuniambia kama alikubaliana na mkewe na wala sikumuuliza kwa nini hakunishtua wakati wanapita Ipogoro. Niliposikia ameuawa, kwa kweli niliumia sana na bado naumia. Kama kweli mkewe alimkatalia kumbe angetii.”
    Marehemu Mwangosi alizikwa Septemba 4, 2012 kijijini kwake, Tukuyu, Wilaya ya Rungwe. Ameacha mjane na watoto wanne. Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.
     chanzo bongo flava blog

    No comments:

    3500K