• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, August 30, 2012

    Tid Aongelea Tuhuma za yeye kutaka kumuua Ally Kiba


    Kwenye Yo heard!!! ya XXL Clouds Fm August 28 2012 Gossip Cop, Soudy Brown aliripoti kwamba kuna mwanamke aliekamatwa na Polisi na kuhojiwa kwa masaa nane wakati akiwa kwenye mipango ya kumuua msanii wa bongo fleva Ally kiba.

    Baada ya kuhojiwa na polisi kwa masaa nane, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ali Kiba.

    Alipohojiwa na Soudy Brown, T.I.D alifunguka na kusema “kwa nini nimuue Ali Kiba bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo, kwa sababu gani?

    Toka nimezaliwa sijawahi kugombana na Ali Kiba, ukibisha muulize mwenyewe kama ameshawahi kukorofishana na mimi, nia ya hao watu ni kuniangusha mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe.”

    Soudy alipomtafuta meneja wa Ali Kiba alijibiwa “hakuna taarifa zozote ambazo ziko tayari kutolewa kwenye vyombo vya habari sasa hivi lakini ikiwa tayari utakua wa kwanza kujua”
    SOURCE

    No comments:

    3500K