• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, August 9, 2012

    Hii ndiyo dunia “Hujafa…hujaumbika”


     
    Beatrice Shimende Kantimbo (48) anaomba msaada wa pesa kwa ajiri ya matibabu ya maradhi ambayo vipimo vya kitabibu vimegundua kuwa ni matende (elephantiasis), ili kufanikisha safari yake kwenda India kwa matibabu.
     
    Kantimbo anasumbuliwa na maradhi hayo kwa takribani miaka 12, kwahivi sasa yamemtoa kwenye mstari wa maisha yake ya kujitegemea na kumfanya awe tegemezi kwa watoto wake na mumewe ambao hata hivyo kipato chao si cha uhakika.
     
    Kabla ya hapo alikuwa ni mama 'mchakarikaji' kweli, aliendesha maisha yake kwa biashara kadhaa ikiwemo biashara ya duka, grosari na saluni ya ususi wa nywele ambapo yeye mwenywe ni msusi mzuri wa nywele na kwa ucheshi wake na kujiamini pia alikuwa akifanya kazi za ushereheshaji (MC) kwenye sherehe kadhaa akifahamika kama MC Kimbaumbau.
     
    Ila kwa sasa, tofauti na hapo awali alipoitwa MC na mama mchakariji, Kantimbo hawezi kufanya lolote amebakia ni mama wa kukaa mahali pamoja tu kuanzia asubuhi hadi jioni.
     
    Kwa uchungu anasimulia namna alivyoanza kuugua…"Nakumbuka mwaka 1998 nikiwa kwenye biashara zangu pale Ubungo, kuna kitu kilinichoma hapa (anaonyesh pajani) maumivu yake yalikuwa mithiri ya sindano, hata hivyo hayakudumu sana wala hapakuwa na alama yoyote.
     
    "Baada ya dakika chache nikajihisi homa kali. nikaanza kutetemeka mwili mzima, nikaamua kwenda hospitali ya Neema, hospili ya karibu na mahali nilipokuwa nikiishi pale Ubungo. Daktari akanipima, akagundua nilikuwa na malaria.
     
    "Wakati huo mguu haukuonyesha dalili zozote za maumivu wala jeraha. Malaria ilkuwa kali, nikalazwa kwa muda wa wiki mbili pale hospitali. Nikaruhusiwa, nikarudi nyumbani na hapo ndipo nilipoanza kuona mguu unavimba. Kaadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo mguu nau unavimba"
     
     
    Kuanzia mwaka 2010 mguu umezidi kuongezeka  kuvimba na maumivu makali yaliyotokana na kidonda kikubwa kilichosababishwa na kuondolewa kwa sehemu ya nyama ya mguu wake wa kuume iliyokuwa imeoza. Anasema:
     
    "Baadhi ya madaktari wa Muhimbili walinishauri nikubali kukatwa mguu. Wanasema ya nyama imeoza na mfupa wa mguu umeharibika. Mimi sikukukubaliana na ushauri wao kwa sababu baada ya kupigwa X-ray 2007 iligunduliwa tatizo kubwa lilikuwa matatizo kwenye mishipa ya kupitisha maji kutokana na nyama kuharibika. Sio mfupa.
     
    "Nilikataa kwa imani kuwa nitapona tu. Nikijiangalia nina uwezo wa kusimama na kutembea isipokuwa tu kinachonipa taabu kwa sasa ni nyama za mguu zimekua sana kiasi kwamba nikitembea zinagusa mguu wa kushoto" alisema.
     
    Kwa mawasiliano namna ya kumsaidia piga simu namba 0716 850350, 0784 861031.

    No comments:

    3500K