meneja uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud
Boniface Meena SHIRIKA
la Umeme Tanzania(Tanesco), limesema ifikapo kesho litakuwa
limeshawaunganishia umeme wateja wake wote walioomba kupata huduma hiyo
kwa muda mrefu.
Hayo yalisemewa jana na meneja uhusiano wa
Tanesco, Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam.
Alisema kwa sasa shirika hilo lina vifaa
vya kutosha na kwamba ndicho kitu ambacho kilikuwa kikiwakwamisha
kutekeleza majukumu yao. “Mteja wetu yeyote ambaye ameomba anapaswa kuwa ameunganishiwa umeme ifikapo Juni 30, mwaka huu,”alisema Badra.
Alisema
wateja ambao walikuwa wameomba wafike katika ofisi za Tanesco katika
maeneo yote zilizopo ofisi zao ili waweze kupatiwa huduma hiyo.
“Tutatoa
namba maalum ili wateja ambao watakuwa wanasumbuliwa na wafanyakazi
wetu waweze kutupigia moja kwa moja na sisi tutashughulika nao,”alisema.
Alisema
hakuna mfanyakazi wa Tanesco anayepaswa kumzungusha mteja wa shirika
hilo hivyo mteja yeyote atakayezungushwa awasiliane na makao makuu ili
waweze kushughulikiwa.
Katika hatua nyingine Tanesco imesema wanatarajia kuzindua mtambo wao mpya wa megawati 100 unaoiwa Jacobsen.
Badra alisema mtambo huo utazinduliwa kesho na kwamba ongezeko la megawati hizo 100 utafanya nchi iwe na megawati 800 za umeme.
|
No comments:
Post a Comment