• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, July 26, 2012

    Linex - Aifola (Official Video)


    July 25 2012 imeingia kwenye kumbukumbu za Mwimbaji Linex kwa kutoa video yake mpya yenye gharama ya zaidi ya milioni 7 za kibongo, ni video ambayo ina kastori nyuma yake na nilikua sifahamu. Video ya Aifola inapoanza kuna Mrembo ambae anaigiza kama mpenzi wa Linex, script ilielekeza Linex ampige kibao huyu mrembo baada ya kukuta msg za mwanaume mwingine kwenye simu yake…. Linex alifanya kweli na kumpiga kibao cha kweli (na sio cha kuigiza) kitu ambacho kilimfanya mrembo akasirike kweli na kuamua kusimama kufanya video. Linex anasema “ilichukua kama saa mbili mpaka tatu kumbembeleza na kukubali kuendelea na shooting ya hii video, nilimpiga akakasirika kweli… nilimpiga kibao cha Serious kabisa haikua kiuigizaji, alipokataa kuendelea kuigiza ilibidi tufanye mambo mengine tu tukisubiri alainike” Video imefanywa na Adam wa Visual Lab, dakika zako nne na sekunde 50 zinakutosha kabisa kuitazama hii video kuanzia mwanzo mpaka mwisho alafu utoe maoni yako, Linex anapita mara kwa mara millardayo.com kuchek ulichomuandikia.

    No comments:

    3500K