V
|
yuo vikuu
60 zikiwemo taasisi za elimu ya juu na wadau wa vifaa mbalimbali vya elimu
kutoka nchi za Afrika mashariki wanatarajia kushiriki katika
maonyesho ya huduma na bidhaa zao yatakayofanyika mwezi ujao mjini
Arusha.
Mratibu wa maonyesho hayo Peter Oguwi amesema
maonyesho hayo yatakayoanza
julai 10 hadi 14 yatafanyika katika viwanja vya nane nane njiro.
Pia yatashirikisha vyuo kutoka nje ya afrika
mashariki ikiwemo India
maonyesho ambayo ameyaelezea kuwa ni ya kipekee na mara ya kwanza kufanyika na
yanatarajia kuleta watu zaidi ya 500.
Oguwi amesema lengo la maonyesho hayo ni kutangaza
huduma zinazotolewa na vyuo hivyo zikiwemo program mbalimbali ilikuwafanya
wananchi wanchi hizo kuthamini vyuo vyao badala ya kukimbilia nchi za nje hivyo
maonyesho hayo yana tarajia kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya
elimu ya juu.
Waziri wa elimu na ufundi Shukuru kawambwa
anatarajiwa kufungua rasmi maonyesho hayo July 11 mwaka huu Jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment