• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Friday, June 22, 2012

    TANZANIA FOOTBALL NEWS: TIMU 20 KUCHEZA LIGI DARAJA LA KWANZA



    K
    amati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeridhia mapendekezo ya Kamati ya Mashindano ya kutaka Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuwa na timu 20 badala ya 18 za sasa.
     
    Lengo la mabadiliko hayo ni Ligi ya Taifa (NL) kuchezwa kwa kanda, hivyo msimu huu timu mbili zaidi (ukiondoa tatu ambazo zimeshapanda kutoka NL) zitaongezwa ili kufikisha idadi ya timu 20 katika FDL.
     
    Timu ambazo zimepanda kutoka NL iliyochezwa katika vituo vitatu ni; Kanembwa JKT ya Kigoma iliyoongoza Kituo cha Kigoma, Ndanda SC ya Mtwara iliyoibuka kinara Kituo cha Mtwara na Polisi Mara iliyokamata usukani katika Kituo cha Musoma.
     
    Kamati ya Utendaji pia imepitisha mapendekezo ya kuchezwa play off ili kupata timu mbili zaidi za kucheza FDL msimu huu. Timu zitakazocheza play off katika utaratibu utakaotangazwa baadaye na Kamati ya Mashindano ni tatu zilizoshuka kutoka FDL na tatu nyingine zilizoshika nafasi za pili katika NL kutoka vituo vya Kigoma, Mtwara na Musoma.
     
    Timu tatu zilizoshuka FDL ni AFC ya Arusha, Samaria ya Singida na Temeke United ya Dar es Salaam wakati zilizoshika nafasi za pili katika NL na vituo vyao kwenye mabano ni Kurugenzi ya Iringa (Mtwara), Mwadui ya Shinyanga (Kigoma) na Tessema ya Dar es Salaam (Musoma).
     
    Hata hivyo, timu zitakazoshuka kutoka Ligi Kuu bado zitaendelea kuwa tatu kama ilivyo kwa zitakazopandwa.

    No comments:

    3500K