• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Wednesday, June 27, 2012

    JK KUWA REFA PAMBANO LA WABUNGE SIMBA VS YANGA


    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa refa wa mchezo wa soka kati ya wabunge mashabiki wa Simba dhidi ya Yanga. Mechi ya wabunge hao mashabiki wa Simba na Yanga, inatarajiwa kufanyika Julai 7, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa ni moja ya matukio yatakayopamba Tamasha la Usiku wa Tumaini. Meneja Mkuu wa Global Publishers, wanaoandaa tamasha hilo, Abdallah Mrisho alisema kuwa wameshamuandikia barua JK ya kumuomba awe mgeni rasmi, vilevile awe refa wa mechi hiyo ya wabunge na kwamba matarajio ni mazuri. “Tuna matarajio ambayo ni chanya kuhusu mheshimiwa rais kuingia uwanjani na kuchezesha mechi ya wabunge na kwa kweli hili litakuwa tukio la kihistoria kuwahi kutokea,’ alisema Mrisho

    No comments:

    3500K