Pages - Menu

Wednesday, December 5, 2012

KIPAJI KIPYA KILICHOTOLEWA NA FID Q KUPITIA UJAMAA HIP HOP DARASA


Hicho ndo kichwa kipya na zao la kwanza kabsaa la Ujamaa Hip Hop Darasa lililoanzishwa na msanii wa Hip Hop kutoka Mwanza Fid Q.Msanii ambaye yuko na Fid Q pichani anaenda kwa jina la Picolo tayari amashapata mafunzo na ameshaiva kiasi kuhusu muziki wa Hip Hop ndo maana Fid Q akaamua msanii huyo aachie ngoma yake na video yake pia.Fid Q anasema kuwa anachotaka kufanya ni kuwasaidia wasanii wadogo wenye vipaji ambao wako mtaani wakiosha magari, wakizurura kwa kuwapatia elimu ya muziki, na maisha pia then kuwapeleka studio kwa gharama zake mwenyewe na baadae kutoa album ya pamoja ambayo baada ya mauzo pesa pia zitarudi katika Ujamaa Hip Hop Darasa
SIKILIZA ngoma ya msanii huyo inayoenda kwa jina la 'Mvua ya Mawe'

No comments:

Post a Comment