Pages - Menu

Friday, October 12, 2012

EPL NEWS: FELLAINI KUFANYIWA UCHUNGUZI WA GOTI

Kiungo Maroune Fellaini wa klabu ya Everton anatarajiwa kurudi katika mazoezi siku ya Jumatatu kwa ajili ya kuangaliwa upya majeruhi ya goti.
Itakumbukwa kwamba nyota huyo alipata majeruhi hayo mwishoni mwa juma katika mechi dhidi ya Wigan waliyomaliza kwa sare ya 2-2, katika Ligi kuu ya England.
Mbelgiji huyo ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ubelgiji katika kuwania kufuzu Michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil dhidi ya Serbia na Scotland.
Chama cha Soka nchini Ubelgiji kimesema Fellaini atawasili siku ya Jumatatu nchini England katika klabu yake ya Everton kwa ajili ya kuangaliwa upya.
Taarifa ya Klabu ya Everton imesema atakapowasili juma lijalo atafanyiwa uchunguzi kwa mara nyingine tena pale Finch Farm.

No comments:

Post a Comment