Pages - Menu

Monday, October 29, 2012

BAADA YA DEAR GOD KUFANYA POA KALA ASEMA KUWA ANAFIKIRIA KUTIMIZA MAOMBI YA MASHABIKI WAKE

NEWZ>>>FILEX MMARI 


Msanii anayefanya poa hivi sasa na ngoma ya 'Dear God' amesema kuwa toka atoe wimbo wake wa 'Dear God' amepata maombi mengi kutoka kwa washabiki wangu wakitaka yeye kutoa album.Kala alisema kuwa kutokana na maombi hayo ya mashabiki anafikiria kutoa album yake ya kwanza na si kwaajili ya kufanya biashara bali ni kwaajili ya kuwaridhisha mashabiki
Kala Jeremiah anasema kuwa album hiyo ambayo itakuwa na ngoma zake hata za kipindi cha nyuma kama 'Wimbo wa Taifa', 'Ningekuwa Raisi' na zingine nyingi.Alisema kuwa album hiyo ataiuza mwenyewe na itakuwa ni gharama nafuu ili kila mtu aweze kuipata, "yani kiasi cha pesa ambacho nitakuwa nauza album hiyo kitakuwa ni kwaajili ya gharama ambazo nimezitumia kutengeneza album hiyo", Kala.

No comments:

Post a Comment