Pages - Menu

Thursday, September 20, 2012

HABARI KUTOKA HUKO MBEYA:MHUBIRI KUTOKA KENYA AHUBIRI BILA KIBALI


NA JAIZMELALEO
KATIKA hali ya kushangaza na kusikitisha kuhusu usalama wa wananchi wa Tanzania hususani mkoani Mbeya, Raia wa nchini Kenya Joseph Mbugwa ameingia nchini kinyemela na kufanya mikutano ya hadhara bila kibali cha Polisi wala mamlaka yeyote ya kiserikali.
Hali hiyo imebainika baada ya muda wa wiki tatu sasa raia huyo kuendelea kufanya mikutano yake mahala mbalimbali katika Jiji la Mbeya na nje ya Jiji huku viongozi wanaosimamia masuala ya usalama wakiwa hawajui Raia huyo kama ana kibali cha kuingia nchini na kufanya kazi au la. Chanzo chetu kimezungumza na raia huyo eneo la Mwanjelwa leo asubuhi ambapo amekiri kuwa hana kibali cha kufanya kazi nchini Tanzania. Duru za kiusalama zimeeleza kuwa hata Kamanda wa Polisi wa mkoa Diwani Athumani na wasaidizi wake nao hawana taarifa ya mikutano inayoendelea kwa kuhamakuhama inayofanywa na Mkenya huyo. Hata hivyi imebainika kuwa katika mikutano yake anauza kanda na CD mbalimbali ambazo anadai kuwa zina makala za kifreemasons.
Chanzo chetu kimeshuhudia jinsi ambavyo Mhubiri huyo kutoka nchini Kenya akiwataja wakuu wa idara mbalimbali hapa nchini kuhusu na matukio mabaya ambayo ameyaita kuwa ya utoaji kafara.

No comments:

Post a Comment