KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amesema
kauli iliyotolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ni
nzito, hivyo anajipanga kuijibu.
Dk
Slaa amesema asingependa kuzungumzia kauli hiyo sasa kwa kuwa yuko ziarani
vijijini, lakini ataitolea tamko wakati mwafaka ukifika. Habari ambazo Dk Slaa
mwenyewe jana jioni amethibitisha kwamba atakutana na waandishi wa habari leo
mjini Iringa, lakini hakuwa tayari kueleza kama atazungumzia kauli ya Sitta au
la. Kauli ya Dk Slaa imekuja baada ya vyombo vya habari nchini kumtaka azungumzie
kauli ya Sitta kuwa muda wa Chadema kutawala nchi bado, kwa kuwa chama hicho
hakina viongozi makini wa kufanya kazi za Serikali. Ofisa Habari wa Chadema,
Tumaini Makene amesema mkutano wa Dk
Slaa na waandishi wa habari utalenga kueleza jinsi Chadema kinavyoendesha
Operesheni Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), baada ya kuzuiwa kwa mikutano yake ya
hadhara. Sitta alipokuwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM wa wilayani
Karagwe Mkoa wa Kagera juzi, alisema kuna upungufu mwingi katika safu ya
uongozi ya Chadema, kutokana na kutokuwa na watu wenye uzoefu wa kufanya kazi
za Serikali, badala yake wana baadhi ya watu wenye uzoefu wa kuongoza kumbi za
muziki. Sitta amesema ukimwondoa Dk Slaa, hakuna kiongozi mwingine anayeweza
kufanya kazi ya kukiongoza na kukifanya chama hicho kikubalike kwa umma.
No comments:
Post a Comment