Pages - Menu

Wednesday, June 27, 2012

MGOMO WA MADAKTARI: DR. ULIMBOKA ATEKWA,KUPIGWA NA KUJERUHIWA VIBAYA SANA!!


  Pichani ni Dokta Steven Ulimboka kama anavyoonekana baada ya kuokotwa leo maeneo ya Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam huko Tegeta alikotupwa na watu wasiojulikana baada ya kumteka jana usiku akiwa nyumbani kwake. Kwa maelezo yake mwenyewe alisema kuwa akiwa nyumbani kwake
jana usiku walikuja watu waliodai kuwa wao ni askari ambao walimchukua na kumpakia kwenye gari ndigi isiyo na plate namba na kisha waliekea barabara ya Bagamoyo ambako baadae walimfunga kitammbaa usoni na kuanza kumpiga sana huku wakidai kuwa kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemchoma afe kwani amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu, Kisha baada ya muda walimtupa Dokta akiwa hajitambui mpaka alipookotwa leo na sasa yuko Muhimbili kwa matibabu!!


No comments:

Post a Comment